Tiiba ya babu imeleta maafa makubwa kwa wagonjwa
Chama cha Madaktari nchini (MAT) kimesema tiba inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila, kwa njia ya kikombe kwa ajili ya kutibu magonjwa sugu, imeleta maafa makubwa kwa wagonjwa. Makamu wa Rais wa MAT, Dk. Primus Saidia, alitoa tamko hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana suala zima la magonjwa yasiyoambukiza…