Kuporomoka kwa bei ya mchele kunawaumiza wakulima
Na Anna Atugonza: Kuna msemo unaosema kufa kufaana. Msemo huu ambao unaangalia zaidi faida ya upande mmoja kwa madhara ya upande mwingine, unaonekana kuchukua mkondo katika kilimo cha mpunga mwaka huu. Hali hiyo inatokana na kuporomoka kwa bei ya mchele, ambayo ni faida kubwa kwa mlaji lakini ikiwa ni hasara kubwa kwa mkulima wa mpunga. Wadau katika sekta hii…