Kushindwa kutambua na kushawishi uwapo wa viwanda vidogo vya kisasa vya chini vya majumbani (home based industries), kumekuwa chanzo cha changamoto ya mwendo goigoi wa ukuaji wa uchumi – Maida Waziri
Presentation CBE, Dodoma Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nimefurahi sana kualikwa katika hadhara hii kuzungumza kuhusu ujasiriamali. Wakati nazungumza huo ujasiriamali nitaunganisha na Waraka Maalumu wa ushauri wa kisera kuhusu Viwanda vidogo vya chini vya majumbani ambao niliuwasilisha Serikalini. Waraka huu niliuandika kutokana na uzoefu wangu wa miaka 30 ya ujasiriamali na kwa kuangalia kasi…
