ASKARI WA WANYAMAPORI AMEUWAWA NA MAJANGILI KATIKA PORI LA AKIBA LA MASWA
Dar es Salaam: Wizara ya Maliasili na Utalii inasikitika kutoa taarifa kwa umma kuwa tarehe 03/01/2012 mnamo saa 6.20 usiku, askari wa Wanyamapori aitwaye Dorcas K. Rumbagi alipigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili katika Pori la Akiba la Maswa. Marehemu alifariki njiani alipokuwa akipelekwa hospitali. Mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda Kibara – Bunda mkoani Mara ambako alizikwa…