WATUMISHI WA WANYAMAPORI WAMETAKIWA KUIMARISHA UHIFADHI
Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Khamis Suedi Kagasheki amewataka askari wa Wanyamapori popote waliko nchini kufanya kazi kwa bidii na bila uoga wakati wanapotekeleza kazi zao za kila siku maana mafanikio ya uhifadhi hapa nchini yako mikononi mwao. Aliwaasa watumishi wote wa Idara ya Wanyamapori kuzingatia ushirikiano (team work) ili kufanikisha uhifadhi kwa manufaa ya kizazi hiki na…